Msanii wa Bongo Fleva, Sam wa Ukweli amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Palestina, Sinza jijini Dar Es Salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Chanzo cha kifo chake kimelelezwa na Producer wake Steve kuwa “Sam alianza kuzidiwa toka Jumamosi, tulipomuuliza anaumwa nini alisema ukimwi lakini sio ukimwi wa kawaida bali wa kulogwa”.
Sam, aliwahi kutamba kwa tungo zake zilizomtambulisha katika muziki wa hapa nyumbani, baadhi ya nyimbo hizo ni pamoja na ” Hata kwetu wapo , Sina raha, Samaki na Kisiki “, wimbo wake wa mwisho aliofanya kabla ya mauti kumchukua .

Mwili wa marehemu umepelekwa katika hospitali ya Mwananyamala kuhifadhiwa, na taratibu za mazishi zinaendelea kukamilishwa ili ahifadhiwe katika nyumba yake ya milele.