Wanafunzi wawili wa chuo Kikuu cha Dar Es Salaam pamoja na Dereva wao wamefariki dunia jana jumatatu, katika ajali iliyotokea eneo la River Side, Mabibo ikilihusisha gari la kubebea wagonjwa ( Ambulance ) na lori la mizigo.
Wanafunzi hao walikuwa kwenye gari la wagonjwa ikidaiwa walikua wakipelekwa Hospitali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa na Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ( DARUSO ) imeeleza kuwa Maria Gordian, alikua mwanafunzi wa mwaka wa kwanza chuoni hapo na Steven Sango, alikua mwaka wa pili .
Mwanafunzi mwingine aliyekua kwenye gari hiyo iliyopata ajali ni, Abishai Nkiko hali yake ni mbaya na anapata matibabu Hospitali ya Taifa ya Muhimbili .
” Tuendelee kumuombea apate kupona haraka “, imesema taarifa hiyo .