Moto mkubwa umeibuka Kariakoo katika Mtaa wa Livingstone na Aggrey na unaendelea kuteketeza maduka. Vikosi kadhaa vya Jeshi la uokoaji na zimamoto vimefika eneo la tukio kukabiliana na moto huo unaoendelea kuteketeza jengo hilo la ghorofa ambalo lina maduka mengi katika ghorofa ya chini.

Jitihada za kuuzima moto huo zinafanywa na Jeshi la uokoaji na zimamoto likishirikiana na wananchi waliopo katika eneo la tukio maeneo ya Kariakoo.