Sunday, May 24, 2020
Swahili > Habari picha > Tuzo za ushairi za Ebrahim Hussein

Tuzo za ushairi za Ebrahim Hussein

Tuzo ya Ushairi

Tuzo hizi za ushairi za Ebrahim Hussein zilianzishwa mwaka 2014 ili kuenzi utunzi wa ushairi wa nguli huyo na mwalimu wa ushairi nchini Tanzania Profesa Ebrahim Hussein. Hii ni mara ya tatu kufanyika kwa shindano hilo tangu kuanzishwa kwake.

Zawadi
Shindano hili hutoa zawadi kwa washindi 20 ambapo 17, hupewa vyeti na wengine watatu wa kwanza hupewa vyeti na pesa taslimu. Ambapo mshindi wa kwanza hupewa zawadi ya cheti na pesa taslim kiasi cha Tsh. 2,000,000, mshindi wa pili Tsh. 1,300,000 na cheti. Mshindi wa tatu pia hupata zawadi ya cheti pamoja na pesa taslimu Tsh.1,000,000.

 

Lulu Khaji
Nusura Khaji (21), mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augostine ambae aliibuka mshindi wa kwanza anasomea shahada ya kwanza ya Ualimu katika somo la Historia na Kiswahili.